h
Bila shaka kila
mmoja wetu anatamani kumiliki nyumba yake,na bila shaka wale ambao
wamekwisha jenga wana ndoto za kujenga tena ama kuwashauri ndugu na
marafiki kujenga.
Ujenzi katika
sehemu kubwa ya Tanzania haufuati taratibu na sheria za ujenzi wa
makazi.Zipo sababu nyingi ambazo zinasababisha hili lakini kwa leo
mjadala utajikita katika namna ya kuchagua ramani bora ya nyumba
Ramani ya nyumba
ni dira ambayo ni kazi ya usanifu yenye kuleta picha ya uhalisia
utakaofikiwa na kutarajiwa na mteja.Kazi hii hufanywa na msanifu majengo
amnbaye kwa lugha ya kiingereza huitwa Architect.
Msanifu
husikiliza kwa makini matarajio ya mteja na kuiweka picha ya matarajio
katika mchoro (picha).Watu wengi hudhani kazi ya Architect ni kuchora tu
ramani,na ndio maana wengi hudhani ni jambo rahisi.Ukweli ni kwamba
kazi yake ni kusanifu mawazo ya mteja na kuyaweka kuwa halisi.Kwa maana
hiyo,hii ni fani ambayo huitaji umakini na elimu ya kutosha ili
kuhakikisha anasanifu jengo ambalo litafanya wanaoishi waishi wakiupata
msawazo katika joto,hewa,mwanga na wawe na furaha na kupapenda
wanapoishi.
Baada bya
maelezo hayo sasa tujiulize je,ramani bora inazingatia mambo
gani?Ijulikane kwamba nimejaribu kupitia vigezo vitakavyomfanya kila mtu
aelewe
Kwa wale ambao wana mpango wa kujenga nyumba bora za kisasa,mambo
yafuatayo ni muhimu kuyazingatia unapochagua ramani bora kwa ajili ya
nyumba yako:
Mchoro ukionesha uhusiano uliopo kati ya sehemu moja na nyingine katika eneo (site plan).Picha ni mali ya Nyumba BoraTz |
1.Izingatie
maono ya mteja (client)-client imaginationikiwa na maana,mteja anapaswa
kupata kile anachokipenda na alichofikiri kichwani kwake eitha kwa kuona
ama kwa kutarajia
2.Iwe na uhusiano mzuri kati ya eneo na eneo (mfano sebule na dining,dining na
jiko, sebule na vyumba.
3. Izingatie
matumizi bora ya ardhi kwani ardhini gharama ( iwe na mgawanyo bora kati
ya eneo linalojengwa, eneo amanafasi ya kutembea (circulating space),
eneo la kijana (green
zone)-ama eneo
linalopandwa miti, maua na vingine vyenye kuleta uhai.Ni lazima iepuke
uwepo wa sehemu zisizo na kazi (dead space)
4.Izingatie hewa
na mwanga wa kutosha katika kila eneo linalotumika,nanyumba bora
huzingatia hewa na mwanga wa asili na sio artificial air.(viyoyozi)
5.Izingatie uwepo wa sitiri (privacy) –ihakikishe kila mtumiajianakuwa na uhuru wa kutosha na kuepuka muingiliano
6. Izingatie kuliendeleza eneo, lisiwe mfu kwa maana ya kuliharibu ama kuondoa vitu
vya msingi ambavyo vinafanya ardhi iwe oevu/endelevu
7. Iwe inazingatia kufikika na matumizi kwa watu wa umri wote na maumbile yote mfano wazee,walemavu.
8. Uzingatie
uzuri- iwe inavutia (appealing to eyes) na wakati Fulani mvuto wake uwe
wa kipekee ama mfano mahali inapojengwapo, iwe kioo cha eneo,utamaduni
na mazingira ya eneo.
9.Izingatie
matumizi bora ya maji na nishati,ikihusianisha vema sehemu zinazohitaji
matumizi ya maji (wet areas) na zisizohitaji maji |(dry areas), sehemu
zenye kuhitaji nishati na kutoa nishati-hot areas na hivyo kurahisisha
matumizi bora ya maji na nishati.Na katika zama hizi ambayo dunia
inashuhudia uhaba wa maji na nishati katika nchi za Afrika,ni vizuri
wasanifu majengo waanze kufikiria majengo ambayo ni rafiki katika
matumizi na rafiki wa mazingira
10.Kwa nyumba
ambazo ni za wakazi wengi,ni vema ikazingatia kukuza uhusiano na undugu
mfano kuwe na kibaraza (verandah ya pamoja), sehemu za mapumziko za
pamoja pia,ili kuhakikisha ujamaa na ushirikiano unadumishwa
Kumbuka nyumba
utakayoijenga ni
sehemu ya kudumu ( permanent structures) hivyo ni vizuri ukifahamu
mapema mambo haya kabla ya kujenga kuepuka mkanganyiko wa
kisaikolojia,maamuzi na uchumi.
N:B- Nyakati hizi watu wanapenda nyumba ambazo zinaondoa kabisa uhusiano wa kijamii mfano
ukaribu na
majirani,ushirikiano-nadhani ni wakati sasa wasanifu majengo Tanzania
wafikirie ni jinsi gani kinachoitwa privacy kinavyoathiri ujamaa,enzi za
nyerere fikra ilikuwa watu wanaotumia apartment wapike pamoja,wafue
sehemu moja,lakini kwa sasa watanzania
wanafiki tofauti na labda kwa sababu hatuna falsafa inayoliunganisha taifa